Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa ticket ya CHADEMA kabla ya kuvuliwa Ubunge na Spika Job Ndugai na juzi kati kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), Joshua Nassari amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge kwa mara nyingine katika Jimbo lilelile la Arumeru Mashariki.
July 08 mwaka huu wakati anatangaza kuhamia rasmi CCM, Joshua Nassari alisema >> “Nimeamua kuweka Nchi yangu mbele, Rais Magufuli amefanya mengi makubwa na mabadiliko ambayo nilikua nayataka, siwezi kuendelea kuwa mnafiki… Mwenyekiti nimekuja tuunganishe nguvu hii, tushikamane tuijenge Arusha yetu, tuijenge Arusha mpya”
Baada ya Spika Ndugai kutangaza kumvua Ubunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari March 2019, Jimbo hilo limekuwa chini ya Dr. John D. Pallangyo ambaye pia alikua kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo akichuana na Nassari kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.