Manchester United na Arsenal zinakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan kwa mshambuliaji wa Bologna Joshua Zirkzee, huku Juventus pia ikihusishwa na mchezaji huyo.
Kinda huyo anapendelea kuhamia AC Milan, kwa mujibu wa The Mirror, na huenda akaondoka majira ya joto.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ameonyesha kiwango kizuri kwa Bologna msimu huu kwa kufunga mabao 10 na kutoa pasi nne za mabao katika mechi 28, akiisaidia Bologna kushika nafasi ya nne kwenye Serie A na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
Hata hivyo, Mholanzi huyo anatarajiwa kusonga mbele na kuondoka katika klabu msimu huu wa joto, licha ya kusajiliwa kutoka Bayern Munich chini ya miaka miwili iliyopita.
“Hakuna uhaba wa wahusika wanaotaka kusaini na United, Arsenal na Juventus kati ya vilabu vinavyohusishwa na fowadi huyo mwenye talanta.
Upendeleo wa Zirkzee ni Milan na amewaagiza wawakilishi wake kufahamu hatua iliyopendekezwa.
“