Baada ya uongozi wa Chelsea kumfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Jose Mourinho na nafasi yake kuchukuliwa na Guus Hiddink kama kocha wa muda wa Chelsea, Mourinho ameingia kwenye headlines ya kampeni za kisiasa, mreno huyo ameingia kwenye headlines baada ya kutia neno katika siasa za nchini kwake.
Stori kutoka today.ng zinaeleza kuwa Jose Mourinho amewaomba wareno wenzake wasifanye makosa ya kumchagua kiongozi wamtakaye, lakini Jose Mourinho amewaomba wamchague Marcelo Rebelo de Sousa kama mtu sahihi wa kuwaongoza.
“Kwa mara ya kwanza ndio najitokeza kuonesha namuunga mkono mgombea gani, kwa sababu nafikiri huu ni wakati sahihi kwa Ureno kufanya chaguo sahihi, zaidi ya miaka ya nyuma” >>> Mourinho
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.