Tanzania ni moja ya nchi zilizowahi kushuhudia maafa ya mafuriko, uharibifu mkubwa kuanzia kwenye makazi ya watu, miundombinu pamoja na watu kufariki ni matukio ambayo kila ikitokea mafuriko basi lazima kuwe na stori kuhusu matukio ya aina hiyo.
September 11 2015 watu wa Japan walijikuta wakiingia kwenye tatizo ambalo huenda siku moja kabla hata hakuna aliyedhani kuna kitu cha aina hiyo kingewakuta… mafuriko yaliikumba baadhi ya miji ndani ya Japan ikiwemo Jiji la Miyagi, watu wakajikuta wakipanda juu ya nyumba zao ili kusubiri msaada wa kuokolewa.
Katika Jiji la Joso, wataalam wa masuala ya hali ya hewa wameshauri zaidi ya watu Milioni 3 kuhama makazi yao kutoka na maafa ambayo yametokea… watu saba wamefariki, wengine 15 bado hawajapatikana na wengine 27 walipata majeraha.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos