Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea kutoridhishwa kwake na hatua zinazochuliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji dhidi ya watu waliouziwa viwanda na kisha kuvitelekeza na amemtaka Waziri wa Wizara hiyo Charles Mwijage kuvinyang’anya na kuwapatia wawekezaji wanaoweza kuviendeleza.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo muda mfupi kabla ya kufungua kiwanda cha kuzalisha saruji cha Kilimanjaro kilichopo katika eneo la Maweni Mjini Tanga ambako leo ameendelea na ziara yake ya siku 5 Mkoani Tanga.
Hata hivyo wakati wa hotuba ya Rais Magufuli mkoani Tanga amemuagiza waziri Mwijage kama kuna nchi inazuia Tanzania kuingiza bidhaa zake kwao na Tanzania inabidi izuie kupokea bidhaa kutoka hiyo nchi maana hawezi kuruhusu Tanzania ya upokeaji bidhaa za nje tu.
“Sasa nataka kama wao wanaleta maziwa huku na sisi maziwa yetu tupeleke huko, siku wakizuia maziwa yetu na wao tunazuia maziwa yao siku hiyo hiyo, haiwezekani Tanzania ikawa ni dumping area tunapokea tu ni lazima sasa tubadilike” >>> Rais Magufuli
VIDEO: “Usipofanya kazi hautakula, usipokula utakufa nawaambia ukweli” hii ya JPM leo bonyeza play kutazama full video.