Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Gabriel Pascal Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General).
Kabla ya uteuzi huo Malata alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na anachukua nafasi ya Dkt. Julius Clement Mashamba.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Boniface Luhende kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General).
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Luhende alikuwa Mhadhiri katika Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha DSM na anachukua nafasi ya Gabriel Pascal Malata ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.