Muda mfupi baada ya kusimamishwa kazi na Rais Magufuli Kamanda wa Polisi Wilaya Njombe (OCD), amerudishwa kazini baada ya Mchungaji alieombwa na Rais kufanya sala ya toba kuombea mauaji ya watoto yaliyokuwa yakitokea mkoani humo miezi michache iliyopita.
Rais Magufuli ambaye kabla ya kumsamehe alihoji kama OCD wa eneo hilo bado yupo ilihali aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo akiwa amesimamishwa kazi kwa kushindwa kumaliza mauaji ya watoto kwa wakati.
“Nilimtimua RPC hapa kwa ajili ya mauaji yaliyokuwa yanatokea hapa Njombe, OCD wa hapa bado yupo? Sasa kuanzia leo nasema naye aondoke najua ananilinda hapa lakini naye aondoke haiwezekani waletwe askari kutoka sehemu zingine kufanya operesheni wao wapo tu hapa” Rais Magufuli
Katika hotuba yake JPM akamuita Mchungaji na kumuomba aongoze sala ya toba kuombea mauaji ya watoto yaliyokuwa yakitokea na baada ya maombi hayo akasitisha kumtimua kazi OCD huyo.
“Haya sasa wote tumekuwa wasafi na OCD niliyemsimamisha kazi nimemsamehe na atabaki kufanya kazi hapa,” Rais Magufuli