Kutokea mkoani Kigoma leo July 21, 2017 amefanya ziara yake ya kikazi ikiwa ni pamoja na kuzindua mradi wa barabara ya Nyakanazi – Kibondo pamoja na Kidahwe – Kasulu, Rais Magufuli amezungumza mambo mengi kwenye hotuba yake ikiwemo kodi, barabara, alivyojitoa kwa Tanzania na mengine.
"Tumeibiwa sana madini, tumewaita waje tuzungumze wakichelewachelewa nitafunga migodi yote, mara kumi wapewe Watanzania" – JPM Kigoma
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Kuanzia tarehe 1 mwezi wa 7, 2017 ukibeba mazao hautatozwa ushuru sio kwa gunia tu, hata tani 1 ya gari' -Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Nataka ifike wakati mtu atoke hapa Nyakanazi hadi Dar es Salaam kwa bajaji kwenye lami na hili linawezekana kabisa' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Nilipokea malalamiko ujenzi unakwenda taratibu mkandarasi asinijaribu, mimi kufukuza makandarasi ni kama kunywa chai' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Niwambie ukweli, fedha nyingi zinapotelea serikalini, ndiomana nimezuia semina, posho za ajabu, safari hadi nikupe kibali' – Rais @Magufuli
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Tulipoingia tulikuwa tunakusanya kodi bilioni 800 tukabana tukapata trilioni 1.3, tukibana zaidi tutapata hadi trilioni 3'-Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Tumeondoa tozo katika sekta za mifugo, uvuvi na kilimo ili kutimiza ahadi ya kuwatumikia wananchi' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Na nyinyi wananchi msinyamaze, toeni ushirikiano kuondoa tatizo la ujambazi' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Mkandarasi fanya kazi usiku na mchana barabara hii ya Kibondo – Nyakanazi ikamilike kwa haraka' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
'Waziri wa Fedha hakikisha mkandarasi analipwa haraka ili tumalize mradi huu haraka iwezekanavyo' -Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 21, 2017
VIDEO: “Usipofanya kazi hautakula, usipokula utakufa nawaambia ukweli” hii ya JPM leo bonyeza play kutazama full video.
VIDEO: Beka wa Yamoto Band ashikiliwa na Polisi toka saa 5 asubuhi, aelezea mkasa mzima kwenye hii video hapa chini