Leo June 21, 2018 Rais Magufuli amepokea gawio la Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania{TTCL} la Bilioni 1. 5 na kuzindua upanuzi wa huduma za TTCL, katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Millardayo.com inakusogezea MAAGIZO 10 aliyozungumza na kuagiza Rais Magufuli.
Jambo la kwanza Rais Magufuli amesema “Kupitia mfumo huu wa ‘TTCL video Conference’ nitawasiliana na wakuu wangu wa mikoa kote nchini na Dr. Shein naye ataitumia kuwasiliana na wakuu wake wa mikoa huko Zanzibar ili kupunguza safari za kila mara mikoani”
“Kupitia mfumo huu wa ‘TTCL video Conference’ nitawasiliana na wakuu wangu wa mikoa kote nchini na Dr. Shein naye ataitumia kuwasiliana na wakuu wake wa mikoa huko Zanzibar ili kupunguza safari za kila mara mikoani” -Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/rb0o597pfz
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Pili ni kuhusu Amani ya Nchi “Penye amani kuna biashara, pesa, chakula, ulinzi, uchumi hata dini zitatoa mahubiri mazuri ndipo unapoweza kukemea hata mapepo yakakimbia, pakikosa amani hakuna kukemea. Amani ndio kila kitu” – Rais Magufuli
“Penye amani kuna biashara, pesa, chakula, ulinzi, uchumi hata dini zitatoa mahubiri mazuri ndipo unapoweza kukemea hata mapepo yakakimbia, pakikosa amani hakuna kukemea. Amani ndio kila kitu” – Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/F9xIuz3C7h
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Tatu ni kwa Viongozi wa Ulinzi na Usalama “Naungana na Watanzania wote kuvipongeza vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama, usiku na mchana hawalali kwasababu ya kulinda amani ya watanzania zaidi Milioni 55, endeleni hivyo msikate tamaa. Umma wa Tanzania upo pamoja na nyinyi – Rais Magufuli
“Naungana na Watanzania wote kuvipongeza vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama, usiku na mchana hawalali kwasababu ya kulinda amani ya watanzania zaidi Milioni 55, endeleni hivyo msikate tamaa. Umma wa Tanzania upo pamoja na nyinyi – Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/owmZBkcAId
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Nne ni agizo kwa Taasisi za Serikali kutumia Walinzi kutoka Suma JKT “Niwashukuru kwa kuwapatia ajira vijana wa Suma JKT wengine waige hakuna sababu ya kuajiri walinzi toka nje ya TZ, nina uhakika pale Wizara ya kazi kuna matatizo matatizo, nasema kwa dhati napafuatilia” Rais Magufuli
“Niwashukuru kwa kuwapatia ajira vijana wa Suma JKT wengine waige hakuna sababu ya kuajiri walinzi toka nje ya TZ, nina uhakika pale Wizara ya kazi kuna matatizo matatizo, nasema kwa dhati napafuatilia” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/LYkhFSiSJW
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Tano ni agizo kwa TTCL “TTCL isiwe na kigugumizi katika kukusanya madeni yote kwa wateja, vinginevyo mtashindwa kushindana katika soko” Rais Magufuli
“TTCL isiwe na kigugumizi katika kukusanya madeni yote kwa wateja, vinginevyo mtashindwa kushindana katika soko” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/VkfOmlHgxa
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Sita leo kutoka kwa JPM “Shirika hili lisiwafie mikononi, itawakuwa ni aibu kubwa, haya mafanikio mliyoyapata katika kipindi kifupi ni sehemu tu ya safari ndefu iliyo mbele yenu” Rais Magufuli
“Shirika hili lisiwafie mikononi, itawakuwa ni aibu kubwa, haya mafanikio mliyoyapata katika kipindi kifupi ni sehemu tu ya safari ndefu iliyo mbele yenu” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/uEOwSbEjPE
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Saba ni taarifa juu ya matumizi ya simu nchini “Sekta ya simu inakuwa kwa kasi sana duniani, watu Milioni 40 Tanzania wanatumia simu za mkononi, huku watu Bilioni 5 duniani wakitumia simu” Rais Magufuli
“Sekta ya simu inakuwa kwa kasi sana duniani, watu Milioni 40 Tanzania wanatumia simu za mkononi, huku watu Bilioni 5 duniani wakitumia simu” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/ovvYZwC6HE
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Nane ni ruhusa endapo TTCL itazalisha “Mimi nikisikia siku moja mmezalisha zaidi japokuwa nilishasema hakuna kupandisha mishahara lakini kwa nyinyi mnaozalisha zaidi hata mkipandishwa mishahara ni safi tu” Rais Magufuli
“Mimi nikisikia siku moja mmezalisha zaidi japokuwa nilishasema hakuna kupandisha mishahara lakini kwa nyinyi mnaozalisha zaidi hata mkipandishwa mishahara ni safi tu” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/Bta7Rp9q0w
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Tisa ni maelekezo ya matumizi ya Gawio walilopata “Gawio hili la Bilioni 1.5 likasaidie kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika kusaidia kwenye bajeti ya mwaka huu 2018/19 nchini” Rais Magufuli
“Gawio hili la Bilioni 1.5 likasaidie kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika kusaidia kwenye bajeti ya mwaka huu 2018/19 nchini” Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/Hw8s6Nf4oT
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Jambo la Kumi ni ahadi kwa Vijana “Vijana wakipewa majukumu wanaweza lakini akitaka kuharibu anaharibu kwelikweli, hii ndo sababu ya kuteua vijana ktk nafasi Serikalini, kwa bahati nzuri wengi niliowateua hawajaniangusha ukiondoa wachache, naahidi kuendelea kuwateua ktk nafasi mbalimbali” JPM
“Vijana wakipewa majukumu wanaweza lakini akitaka kuharibu anaharibu kwelikweli, hii ndo sababu ya kuteua vijana ktk nafasi Serikalini, kwa bahati nzuri wengi niliowateua hawajaniangusha ukiondoa wachache, naahidi kuendelea kuwateua ktk nafasi mbalimbali” JPM#MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/WKikREZ0ba
— millardayo (@millardayo_) June 21, 2018
Rais Magufuli ametumia VIDEO CALL kumtaka Waziri Mkuu atoe maagizo