Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi, Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo.
Rais Magufuli amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini MUNGU.
‘Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu’-Rais Magufuli.
‘Nafikiri mnaweza mkaona sura yangu, ni inawezekana inatafsiriwa mtu katili, wa ajabu, siko hivyo, mimi ni mpole, mnyenyekevu, mwenye upendo mkubwa, ninayeogopa dhambi na mwenye hofu ya Mungu lakini ukweli mimi ni mkali kwa maovu’-Rais Magufuli.
Umepitwa na Taarifa ya Habari ya AzamTV leo April 30 2017, Unaweza kutazama kwa kubonyeza play hapa chini