Moja ya stori zilizo make headlines kwenye mitandao ya kijamii kutokea Bungeni Dodoma wiki hii ni ni pamoja na hii ya Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa aliyesimama kuchangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ishu kubwa ikawa ni kwanini Wanaume wengi jimboni kwake hawaoi Wanawake wazuri?
Mapokeo ya baadhi ya watu yakawa tofauti na kupelekea wengine kumkosoa kwa kauli hiyo, AYO TV iemempata Bashungwa na kufanya naye exclusive Interview…
…‘Muda haukutosha bungeni kuelezea hoja yangu, mimi nilizungumzia changamoto katika jimbo langu la Karagwe, hoja yangu ilikuwa kuiomba Serikali iunde tume ya kuhakikisha Ng’ombe ambao sio wa Tanzania walio katika pori la Kimiso wanaondoka ili wananchi wangu wapate maeneo kwa ajili ya kilimo na mifugo. ’
‘Lengo langu haikuwa ni kuwabeza Jeshi la Polisi bali ni kuwa kuna changamoto katika mipaka ikiwemo mahusiano kati ya kambi ya Jeshi na vijiji vinavyowazunguka’
‘Katika kuizungumza ndio nikasema Vijiji vinakuwa na hofu, lakini naelewa kwenye bunge kila kinachoongelewa mule kinakuwa na thamani. Sasa media wakanyanyuka na hilo la Wanaume wa Karagwe wanaogopa kuoa wanawake warembo ’
‘Kwenye siasi kuchukuliwa tofauti ni vitu vya kawaida, watu wanaonifahamu walishtushwa sana lakini walivyopata mchango mzima wakasema huyu ndio Innocent Bashungwa tunaye mfahamu’.
Unaweza kuipata full interview kwenye hii video hapa chini…
ULIIKOSA HII? VIDEO YA MBUNGE INNOCENT BASHUNGWA AKICHANGIA KATIKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE