Tunayo story kutokea kwa Waziri wa Viwanda, Joseph Kakunda ambapo amesema ikiwa ni miaka 100 ya uhusiano baina ya Uingereza na Tanzania, serikali ya nchi hiyo imetoa ahadi mbalimbali kwa serikali ya Tanzania ikiwemo kusaidia huduma za Kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kakunda amesema Balozi wa Uingereza amefika ofisi kwake lengo la kumpongeza baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda pamoja na kumueleza jinsi wafanyabiashara wa Uingereza walivyowekeza nchini na kuajiri Watanzania.
“Tumekubaliana serikali ya Uingereza itaendelea kusaidia katika huduma muhimu za kijamii ikiwemo Maji, Afya, Elimu na Viwanda,“amesema