May 15, 2017 Rais Magufuli alivunja rasmi Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma ‘CDA’ na kuagiza mali na shughuli zote zilizokuwa zinafanywa na Mamlaka hiyo zihamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kuondoa mgongano wa utoaji wa huduma uliosababishwa na vyombo hivyo viwili.
Sasa jana August 28, 2017 Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alikutana na waandishi wa habari Dodoma na kuzungunzia mkakati mpya ulioandaliwa na Serikali kushughulikia taratibu za watu waliouziwa viwanja na wale wanaotarajia kufanya hivyo hivi karibuni.
“Manispaa ya Dodoma ilikabidhiwa jukumu la kuuendeleza Mji Mkuu wa Nchi. Shughuli zote ambazo zilikuwa zinafanya na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu lakini zimekabidhiwa Manispaa ya Dodoma.
“Ni kweli kuna sintofahamu kwa Wananchi kwamba nini kinaendelea. Nitatoa habari kuwafahamisha Wananchi wa Manispaa ya Dodoma na Watanzania kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma tumeshachukua shughuli zote za CDA na tunaendelea kuzitekeleza kama kawaida.” – Godwin Kunambi.
ULIPITWA? Rais Magufuli aivunja Mamlaka ya Ustawishaji CDA…tazama kwenye video hii hapa chini!!
ULIKOSA? TUNDU LISSU APINGWA: Wakili Manyama kaongea hadharani
MBUNGE MSUKUMA: Kamjibu tena Lissu kuhusu mgomo wa Mawakili