Baada ya miaka tisa kwa mara ya kwanza msimu wa 2018/2019 wa Ligi Kuu Hispania maarufu kama LaLiga ndio tutashuhudia mchezo wa kwanza wa El Clasico ukizikutanisha timu za FC Barcelona dhidi ya Real Madrid bila uwepo wa Cristiano Ronaldo.
El Clasico ya msimu wa 2018/19 itamkosa Ronaldo kutokana na staa huyo kuhama timu na kujiunga na Juventus ya Italia akitokea Real Madrid, muwakilishi wa LaLiga nchini Tanzania Sami Hanane ameongea na waandishi wa habari na kuweka wazi hilo.
Sami amethibitisha kuwa haoni sababu ya El Clasico kupoteza mvuto kwa sababu ya kuondoka kwa Ronaldo, Real Madrid anaamini inaweza kufanya vizuri bila Ronaldo “Kwa upande wangu naona El Clasico itafanya vizuri bila Ronaldo kwa sababu Real Madrid watataka kuthibitisha kuwa wanaweza kufanya vizuri bila Ronaldo”
Haji Manara haishiwi maneno “Kabla ya kunitolea povu nipinge kwa data”