Timu za Tanzania Mtibwa Sugar na Simba Sports Club zinakabiliwa na mechi za Kombe la Shirikisho Barani Afrika na Ligi ya Mabingwa zitakazochezwa Jumanne Novemba 27,2018 na Jumatano Novemba 28,2018.
Mtibwa Sugar wanacheza na Northern Dynamo ya Shelisheli Kesho Jumanne saa 10 jioni Azam Complex,Chamazi, mchezo huo utachezeshwa na Waamuzi kutoka nchini Zimbabwe, mwamuzi wa kati Pilan NCUBE, mwamuzi msaidizi namba 1 Edgar RUMECK, mwamuzi msaidizi namba 2 Tafadzwa NKALA, mwamuzi wa akiba Nomore Murambiwa Musundire, Kamishna wa mchezo Anatokea Rwanda Gaspard Kayijuka
Mchezo wa Simba dhidi ya Mbabane Swallows utachezwa Jumatano Novemba 28,2018 saa 10 jioni Uwanja wa Taifa, mchezo huo utachezeshwa na Waamuzi kutoka Burundi, mwamuzi wa katikati Pacifique NDABIHAWENIMANA,Mwamuzi msaidizi namba 1 Willy Habimana,Mwamuzi Msaidizi namba 2 Gustave Baguma,Mwamuzi wa akiba Georges Gatogato,Kamishna wa mchezo anatokea Zambia Joseph Nkole.
IMETOLEWA NA TFF
Watanzania waishio Afrika Kusini wamejipanga kuelekea Lesotho leo