Mfanyabishara Yusuf Manji amekamata tena headlines leo August 10, 2017 baada ya upande wa Serikali kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itafika na mashahidi wasiozidi 10 katika kesi ya kutumia na kujihusisha na dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara huyo.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya kumsomea Manji maelezo ya awali (Ph) ambapo katika maelezo hayo, Vitalis amedai mshtakiwa ni mkazi wa Sea view DSM, pia ni mfanyabiashara anayetuhumiwa kujihusisha na kutumia dawa za kulevya.
Amedai kuwa alikamatwa February 2, 2017 kisha akapelekwa kituo cha Polisi ambapo alichukuliwa hadi nyumbani kwake na kupekuliwa na baada ya kupekuliwa alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kuchukuliwa haja ndogo (Mkojo) ambao ulipimwa na kukutwa na dawa za kulevya aina ya Benzodiazepine.
Baada ya kusomewa maelezo hayo, Manji alikubali wasifu wake kwamba ni mfanyabiashara, makazi na jina lake licha ya kudai limekosewa ila usahihi ni Yusufali Manji huku akikana maelezo mengine.
Aidha, wakili Vitalis ameieleza Mahakama kwamba wanaomba kupangiwa tarehe kwa ajili ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, pia wanatarajia kuwa na mashahidi wasiozidi 10 hivyo Hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi August 22, 23, na 24, 2017 kwa ajili ya kusililizwa mfululizo.
Manji amkataa Wakili Kibatala kusimamia kesi yake…kisa? Tazama kila kitu kwenye video hii hapa chini!!
VIDEO: Yusuph Manji alivyotolewa Hospitali na kupelekwa Mahakamani, play hapa chini kutazama kila kitu!!!