Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane Ijumaa ya July 5 2019 alikuwa uwanjani kulipambania taifa lake dhidi ya Uganda na kuipatia ushindi wa goli 1-0 alilolifunga dakika ya 15, hata hivyo Sadio Mane dakika ya 60 alikosa mkwaju wa penati kufikisha jumla ya idadi mbili ya penati alizokosa kati ya tatu alizozipiga katika mechi mbili zilizopita.
“Kiukweli walikuwa imara sikuona timu kama wao walikuwa imara na kuweza kushambulia, hivyo haikuwa rahisi kucheza mpira wetu kama ilivyokuwa siku zote Uganda ni timu nzuri, kuhusu penati ingekuwa bora kuongoza kwa 2-0 lakini nilijisikia vibaya kukosa ila nafurahi tumefuzu lakini nafikiria wakati mwingine nitmpata penati apige mwingine atakayeweza kufunga”-Sadio Mane
Baada ya ushindi huo Senegal sasa watacheza dhidi ya Benin katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo, Benin ambao wamepita kwa njia ya Best Looser kuingia hatua ya 16 bora na baadae kuitoa vigogo Morocco kwa mikwaju ya penati 4-1, hiyo ni baada ya mchezo huo kuchezwa na kumalizika kwa dakika 120 wakiwa sare ya 1-1.
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?