Mama na binti yake wamehitimu Chuo Kikuu kimoja na siku moja ambapo kutokana na kufanana kwao wengi walishindwa kuwatofautisha huku wakijua ni mtu na dada yake licha ya kuwepo kwa tofauti ya miaka 35 baina yao.
Suzanne Isaac mwenye umri wa miaka 57 ambaye ni mama wa watoto wawili anaonekana kufanana sana hadi maumbile na binti yake Melissa Isaac mwenye umri wa miaka 22, alianza kusoma masomo yake kama mwanachuo wa ‘Part Time’ katika Chuo Kikuu cha Swansea wakati binti yake akiwa na miaka 16 na hakutegemea kama wangeweza kuhitimu siku moja.
>>>”Watu wengi wanasema mimi ni dada yake Melissa kwangu ni suala zuri maana naonekana mdogo kuliko umri wangu, na ninafurahi kwa sababu tuna asili ya kuwa na miili ya kutozeeka mapema.” – Suzanne Isaac.
ULIPITWA? Ripoti ya Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ kuhusu Uchunguzi wa uvamizi wa Clouds Media Group…play kutazama!!!!