Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaendelea na maandalizi yake ya mchezo wa kuitafuta tiketi ya kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2019 AFCON 2019 itakayochezwa nchini Cameroon, Stars inajiandaa dhidi ya Lesotho kucheza Novemba 18,2018 Maseru,Lesotho.
Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka Tanzania TFF ni kuwa katika mazoezi hayo ya leo golikipa Beno Kakolanya na mshambuliaji Yahya Zayd walipumzishwa baada ya kugongana, taarifa ya madaktari baada ya kuwafanyia uchunguzi wachezaji hao wataendelea na mazoezi kuanzia kesho.
Wachezaji wanaocheza nje wataanza kuripoti kambini Jumapili November 11,2018, wanaotarajiwa kuanza kuripoti ni Ramadhan Kessy (Nkamia,Zambia), Himid Mao (Petrojet,Misri), Rashid Mandawa(BDF,Botswana) na Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini), Waliobaki wataripoti kuanzia November 12,2018.
IMETOLEWA NA TFF
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19