Mchezaji Juan Mata anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo kujiunga na klabu ya Manchester United baada ya Chelsea kukubali kumuuza kwa ada ya uhamisho ya £37m.
Club za Manchester United na Chelsea zimekuwa katika mazungumzo ya usajili wa mchezaji kwa takribani siku mbili zilizopita, na jana usiku ripoti zilitoka kwamba wamekubaliana ada ya usajili na mchezaji huyo angefanyiwa vipimo leo hii jijini Manchester kabla ya kusaini kusaini mkataba wa miaka minne na nusu wa kuwepo Old Trafford.
Mata ambaye alikuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa miaka miwili iliyopita, jana alifanya mazoezi ya peke yake wakati wachezaji wenzie wakijiandaa na mchezo wa FA Cup dhidi ya Stoke City, pia aliwaaga wenzie na kuwaambia kwamba anajiunga na Manchester United.
Usajili wa Mata endapo utakamilika baada ya kufaulu vipimo basi utavunja rekodi ya ada ya usajili wa klabu hiyo ya Manchester ambayo waliiweka baada ya kumsajili Dimitar Berbatov kutoka Spurs kwa ada ya £30.75m September 2008.
Hii tweet ya Rio hapa chini ilitoka saa kadhaa kabla ya hii stori hapa juu