Mshambuliaji wa Real Madrid, Jude Bellingham amefungiwa mechi mbili kufuatia hasira yake dhidi ya mwamuzi katika mchezo dhidi ya Valencia.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikasirishwa sana baada ya mwamuzi, Gil Manzano, kushindwa kutoa bao hilo mara tu filimbi ya mwisho ilipopulizwa Jumamosi Machi 2, 2024.
Kwa mujibu wa Bellingham, filimbi ilipigwa huku mpira ukiwa hewani na langoni. ilitakiwa kuwa goli.
Manzano alieleza katika ripoti yake rasmi ya mwamuzi kwamba alitoa kadi nyekundu kwa sababu Bellingham “alinikimbilia kwa ukali na kupiga kelele, akirudia mara kadhaa, ‘Ni bao la mfalme!'”