Kijana mmoja mjini Cairo, nchini Misri aliyekuwa na silaha za moto ameingia kanisani na kuanza kupiga risasi waumini huku ibada ikiendelea, ambapo ameuwa watu tisa kwa mkupuo huku akijeruhi wengine akiwemo askari polisi.
Inaelezwa hili ni tukio kubwa kwa siku za hivi karibuni la kigaidi kutekelezwa likiwa ni la kiimani na kwamba askari walifanikiwa kumtia nguvuni huku na yeye akiwa na majeraha ambapo amekutwa akiwa na risasi pamoja na bomu alilotaka kulilipua kanisani hapo.
Nchini humo kumekuwa na mashambulio mbalimbali yanayounganishwa na imani za kidini ambayo yamechukua uhai wa Wakristo wengi kwa mwaka mmoja uliopita na wanaotekeleza mashambulio hayo wameendelea kutishia kufanya mengine.
Agizo la Waziri Nchemba kama huna kitambulisho cha utaifa
“Kwenye kupiga rungu siangalii mtu usoni” -Juliana Shonza