Leo March 24, 2018 moja ya stori ninayokusogezea ni kumhusu President Muhammadu Buhari wa Nigeria ambapo amewapokea wasichana 106 waliochiwa huru na kundi la kigaidi la Boko Haram hivi karibuni.
Wasichana waliwasili mapema kwenye makazi ya President Buhari wakiwa na afya njema, japokuwa kuna wanne ambao imeelezwa kuwa walivunjika miguu.
Walisafirishwa kwa ndege mpaka mjini Abuja siku ya Jumatano ambapo walitakiwa kwenda kufanya uchunguzi hospital na na katika vituo vya usalama baada ya kukabidhiwa kwa mamlaka za kiraia.
Buhari amewataka wasichana waendelee kutimiza ndoto zao bila kuogopa machafuko, amevitaka vyombo vya ulinzi kuhakikisha usalama unakuwepo kwenye shule zote zilizo hatarini kushambuliwa na kuonya kuwa iwapo tukio hilo litatokea tena hatalichukuliwa kirahisi.