Utaratibu mpya bungeni ni wa timu maalum iliyopewa kazi maalum ya kurekodi matukio ya Bunge yote yanayofaa kufikishiwa Wananchi na hayo matukio ndio wanapewa waandishi wa habari ila hakuna tena utaratibu kama wa zamani kwamba kila mwandishi anaweza kurekodi kwa Camera yake chochote anachoona ni habari.
April 24 2016 Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania ‘JUHWATA’ limetoa tamko la mwenendo wa shughuli za bunge ambapo limeiomba Serikali kama wameamua kuzuia bunge kutoonyeshwa pia waache kuonyesha maswala yao ya Kiserikali kuweka usawa na kutoonyesha bunge na badala yake muda huo wananchi wakafanye kazi za kujiingizia kipato badala ya kuangalia vipindi vya live, mbele ya waandishi wa habari kupitia katibu wa Jukwaa hilo, Mtela Mwampamba wameyazungumza haya……….
>>>‘tunaposema kwamba Bunge lisionyeshwe live kwa sababu wananchi wanatakiwa wawe kazini na serikali pia masuala yao ya kiserikali kama ufunguzi wa daraja, ufunguzi wa Mwenge yasionyeshwe nayo live tusubiri yarekodiwe ili wananchi waendelee kufanya kazi, kama wanaonyesha live labda iwe sikukuu ya kitaifa’:-Mtela Mwampamba
Aidha Jukwaa hilo limezungumzia tabia ya baadhi ya wabunge kususia mijadala, vikao na shughuli nyingine za bunge kwa kuwa wamekuwa wakivunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara 63 (2) inayozungumzia uwezo wa bunge na majukumu ya bunge wamesema……
>>>’tabia hii ya kuendelea kususa inatunyima fursa sisi wananchi wa kawaida kuweza kujua mawazo mbadala, tumekuwa tunapata mawazo ya upande mmoja kwa sababu upande wa pili umekuwa na tabia ya kususa’ :-Mtela Mwampamba
ULIIKOSA SABABU ZA UKAWA KUSUSIA BUNGE LA BAJETI? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE