Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda leo Mei 8, 2024 amewasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Bungeni Mkoani Dodoma.
“Idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika Vyuo vya Ufundi na Amali imeongezeka kutoka Wanafunzi 171,581 na kufikia Wanafunzi 235,804 na hii imetokana na kuongezeka kwa idadi ya Vyuo vya Ufundi na Amali”- Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
“Jumla ya Wanafunzi 22,131 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wamesajiliwa kwa ajili ya kupatiwa Elimu ya Sekondari katika vituo vya kutolewa Elimu ya Watu wazima”- Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
“Serikali imetoa mafunzo kwa Wanafunzi 376 ambari kwa Mafunzo ya Uanagenzi Wanafunzi 195 na Wanafunzi 181 katika mafunzo ya Umeme wa Viwandani, nishati ya Jua Ufundi majokofu, na Utayarishaji wa Vyakula”- Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda