Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan, ameziomba Jumuiya na Taasisi za Kidini Nchini kujitolea kusaidia kuandikisha Watoto wanaojiunga na darasa la kwanza mwakani 2024, ili kupunguza idadi kubwa ya Watoto waliojitokeza kujiunga na elimu hiyo mwakani katika shule za serikali.
Kauli hiyo ameitoa mwisho mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa Tuzo za 17 za Rais za Wazalishaji wa Viwanda Nchini, zilizoandaliwa na Shirikisho la Viwanda hapa nchini (CTI).
Rais Dk, Samia alisema kuwa katika kukabilina na upungufu wa madarasa katika shule za serikali, ameziomba Taasisi na Jumuiya hizo kujitolea na kumuunga mkono katika jitihada zake za kuhakikisha kila mtoto hapa nchini mwenye sifa ya kujiunga na elimu hiyo anapaswa kuipa kwa njia yoyote ile.
“Ana amini kuwa kupitia Taasisi na Jumuiya hizo kwa pamoja bila ya kujali Dini gani Watoto hao, kwa kupitia huko watapata mafunzo na elimu bora ya darasani na mafunzo ya dini na kuwafanya Watoto hao kuwa na maadili mema na uzalendo kwa nchi yao”, alisema Rais Dk. Samia.
Aidha, alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia sana kuondoa tatizo la Watoto kukosa nafasi za kujiunga na elimum ya msingi mwakani, ambayo ni haki ya msingi kwa kila mtoto hapa nchini kuipata kwani ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ya mwaka 2020 mpaka 2025.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Sunni Muslim Jamaat Muhammad Waseem, alisema kuwa kama jumuiya hakuna zaidi ya kusaidia jitihada za Rais wa Awamu ya Sita Dk, Samia Suluhu Hassan, kwa vitendo na wapo tayari kumuunga mkono katika jitihada zake hizo za kuhakikisha Watoto wote wenye sifa wanajiunga na elimu ya msingi mwakani.
Waseem alisema kuwa kwa kuanzia Jumuiya hiyo imeanzisha shule ya Awali na ya Msingi iliyopo mtaa wa Mindu Upanga jijini Dar es Salaam ambayo inauwezo wa kuchukuwa zaidi ya wanafunzi 500 mpaka 600, ambao itapunguza sana tatizo la upungufu wa watoto kukosa nafasi za kuanza shule ya msingi mwakani.
Aidha, Waseem alisema kuwa licha ya kuwaandikisha Watoto kujiunga na shule zao, bali pia watapata fursa nyingie ya kupatiwa Bima ya Afya itakayo tolewa na Jumuiya hiyo kama msaada kwa Watoto hao watakao jiunga na shule zao ili kuboresha afya zao Pamoja na kupa elimu bora.
“Jumuiya yao imejipanga vizuri kusaidia serikali ya Rais Dk, Samia ambayo imeonyesha kuthamini na kujali Taasisi na Jumuiya za kidini hapa nchini kuwa zinamchango mkubwa katika kusaidia maendeleo ya kielimu, Afya na Uchumi”, alisema Waseem.
Waseem alisema kuwa shule za Jumuiya hizo zinatoa elimu bora bila ya kubagua dini, Kabila wala dhehebu lolote na wanapokea Watoto wote kwa ajili ya kupata elimu.