Meneja anayeondoka Liverpool, Jurgen Klopp amekataa kufikiria kuchukua mikoba ya Bayern Munich kufuatia uamuzi wa Thomas Tuchel kuondoka klabu hiyo mwishoni mwa msimu.
Klipp alikuwa ametangaza mapema mwaka huu kwamba angeondoka Liverpool msimu huu wa joto ili kuchukua muda wa nje na kutumia wakati zaidi na familia yake.
Katika taarifa ya mshtuko kwa mashabiki wa Liverpool, Klopp alitangaza kuwa ‘anaishiwa na nguvu’ katika nafasi yake kama meneja na ataondoka Reds mwishoni mwa msimu.
Meneja huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alisema kuwa hana hamu ya kuinoa tena Ligi ya Premia kwa sababu ya kuvutiwa na Liverpool. Pia amegoma kuzungumzia uwezekano wa kuisimamia timu ya kimataifa.
Kulingana na Daily Express, wakala wake Kosicke aliambia Sky Sports Ujerumani: “Jurgen Klopp hatafundisha klabu yoyote au timu ya taifa kwa mwaka mmoja baada ya msimu huu wa sasa. Hilo bado halijabadilika.”
Muda wa Klopp akiwa Liverpool umekuwa wa mafanikio.
Mjerumani huyo alishinda kila kitu katika klabu ya Merseyside ikiwa ni pamoja na, Ligi ya Premia, Ligi ya Mabingwa ya UEFA, Kombe la FA, Kombe la Carabao na wengine wengi.