Ni Usiku wa kuamkia July 19,2024 ambapo Staa kutokea Bongo Flevani Juma Jux ameonekana na binti wa staa wa Nollywood, Iyabo Ojo aitwae Priscilla Ajoke Ojo wakiburudika katika chimbo liitwalo Elements Masaki jijini Dar es Salaam.
Bado haijajulikana kama wawili hao kama wapo kwenye mahusiano lakini Ayo TV Entertainment inakuahidi tutamtafuta Jux kueleza kwa kina kuhusu ukaribu wake na mrembo huyo.