Staa wa Tottenham Hotspurs anayeichezea timu ya taifa ya Ivory Coast baada ya kutolewa AFCON Serge Aurier, aliongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa haikuwa malengo yao kuishia hapo walitamani kwenda mbele zaidi ila ndio hivyo bado wana kikosi kichanga ambacho kinajengwa chini ya kocha Ibrahim Kamara.
Ivory Coast hawajatwaa taji la AFCON toka 2015 walivyotwaa kwa mara ya mwisho, kwa sasa baada ya kuondoka kwa kizazi cha dhahabu cha kina Toure, Drogba na Kalou wanaamini huu ni wakati wao wa kujenga upya kikosi chao, hiyo ni baada ya kupoteza mchezo kwa penati 4-3 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.
Baada ya penati ya ushindi ya mchezaji wa Ivory Coast kucheza waandishi wa habari wa Algeria walioyokuwa Media Stand walimwaga machozI kwa furaha wakiwa hawaamini kilichotokea, Algeria wanaamini huu ni mwaka wao na wanaweza kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 29 (1990).
VIDEO: Mtangazaji wa Ennahar TV amwaga machozi Algeria ikitinga nusu fainali AFCON