Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) wakishirkiana na Kampuni ya YONO leo May 30 2018 imewatembelea wadeni wote ambao wanadaiwa na shirika hilo na kutoa agizo kwa ambao watashindwa kulipa madeni mali zao zitapigwa mnada .
Kaimu Meneja wa SIDO Dar es salaam Baraka Kandonga amesema madeni ya nje wanayodai ni zaidi ya sh. Mil 200 ikiwa ni wateja zaidi ya 54 ambao watawafikia na kila mtu atachukuliwa hatua kwa ambae hatalipa .