Kwenye Magazeti ya Tanzania leo July 26, 2017 moja ya issue iliyomake headline ni pamoja na hii ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete kueleza kusikitishwa kwake na kasi ya vifo vya uzazi licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali.
Tayari nimekukusanyia stori zote kutoka kwenye twitter yangu ya @millardayo na kukusogezea hapa kupitia millardayo.com.
RPC Pwani, Jonathan Shana ametangaza mapambano dhidi ya wahalifu na kuahidi kuwasaka popote ili kuhakikisha usalama ktk Mkoa huo. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Mtu mmoja ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kujaribu kuiba pikipiki katika Kitongoji cha Amani, Kerege, Bagamoyo. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 Jakaya Kikwete ameeleza kusikitishwa na kasi ya vifo vya uzazi licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Imeelezwa watumiaji vibaya wa mitandao ya kijamii watabainika kirahisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa msaada wa China. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Mkazi wa Sagara Ubungo, Yuda Ramadhani (18) amefikishwa Mahakamani Kinondoni, DSM akituhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 15. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Diwani wa Kata ya Moita, Monduli, Simon Sapunyu (CHADEMA), amejiuzulu wadhifa wake akidai kuvutiwa na utendaji wa Rais Magufuli. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Polisi DSM inawashikilia watu 2 kwa uchunguzi wa kipolisi ktk tukio la kudaiwa kubakwa na kunyongwa hadi kufa mtoto wa miaka 11. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Rais Magufuli amesema hatotetereka ktk jitihada zake za kutetea na kulinda rasilimali za nchi na kuwataka WaTZ kumuunga mkono. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Spika Ndugai amekiri kupokea na anaitafakari barua ya M/kiti wa CUF Prof. Lipumba ya kuwavua uanachama wabunge 8 na madiwani 2. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Waziri wa Utalii Prof. Maghembe amewaomba Mabilionea 26 waliozuru Tanzania kuwa mabalozi wa amani ili kuwanusuru wanyamapori. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imeahirisha kusikiliza mapingamizi matatu ya Serikali ktk kesi ya bomoabomoa Kibamba. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Polisi Arusha imefanya ukaguzi wa kushtukiza kati ya Julai 22 na 24 na kukamata mabasi 77 kwa makosa ya mwendokasi na ubovu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Wanandoa, mtumishi wao wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa ktk ajali ya gari Kisolanza, wakati wanakwenda kwenye mazishi. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Viongozi 51 wa CHADEMA wapo mahabusu ktk gerza la Biharamulo, Kagera baada ya kukosa dhamana ktk Mahakama ya Wilaya ya Chato. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Rais Magufuli amesema baadhi ya hatua ilizochukua Serikali ktk ubinafsishaji miaka ya nyuma zimewaumiza WaTZ badala ya kuwasaidia. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Waziri Mwalimu ameagiza kusimamishwa kazi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mlandizi kwa kushindwa kusimamia maelekezo ya Serikali. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jenerali Mabeyo amesema Jeshi litaendelea kuwaenzi mashujaa, wastaafu na linathamini mchango wao. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Serikali imejidhatiti kukabiliana na biashara utoroshwaji wa madini katika maeneo ya migodi, viwanja vya ndege,bandari na mipakani. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Jeshi la Polisi limesema kukamata wanasiasa au viongozi wa dini sio kwa sababu za kichama au kidini bali ni kwa sababu ya uhalifu. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Serikali wilayani Tunduru, Ruvuma imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria walimu ambao watatajwa kujihusisha kimapenzi na wanafunzi. #Majira
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Vikundi 137 vya Ujasiriamali katika mikoa ya Lindi na Mtwara vimepatiwa Tsh. Bilioni 1.76 na Benki ya Posta ili kuwezesha mitaji. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imevifutia udahili wa Wanafunzi 2017/18 vyuo 19 na kufuta kozi 75 ktk vyuo 20 kwa kukiuka Sheria. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Serikali imewakataza watoa huduma za tiba asili na mbadala kutangaza dawa ambazo hazijasaliwa kisheria na Baraza la Tiba asili. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) kimeiomba Serikali iondoe kodi ya Bajab zinazotumiwa na watu wenye ulemavu kama miguu. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Rais Magufuli amezindua Uwanja wa Ndege mpya Tabora wenye uwezo wa kutua ndege kubwa zinazoweza kubeba abiria 80 au zaidi. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 26, 2017
Agizo Rais Magufuli amelitoa kwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS…play kwenye VIDEO hii kutazama!!!