Mshambuliaji wa zamani wa Man United ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani Javier Hernandez Chicharito, amerudi tena kwenye headlines baada ya kumzungumzia kocha wa Man United Louis van Gaal.
Chicharito aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa alijitahidi kadri ya uwezo wake na angependa kuendelea kusalia Man United lakini Louis van Gaal hakuweza kumpa nafasi licha ya kuonesha jitihada, hivyo ikamlazimu aondoke Man United akitokea Real Madrid kwa mkopo na kujiunga na Bayer Leverkusen.
Staa huyo wa kimataifa wa Mexico alipewa nafasi ya na Sky Sport ya kumzungumzia kocha huyo ambaye kwa sasa hafanyi vizuri sana ndani ya klabu ya Man United na huenda akatimuliwa mwisho wa msimu kama ambavyo anaripotiwa na magazeti mengi ya Uingereza, alitumia mistaa
“Kiukweli ni kocha mzuri ana mbinu za kipekee kama walivyo makocha wengine duniani, huwezi kumpata Sir Alex Ferguson mpya katika miaka 50 au 100 ijayo kwa sababu yeye alikuwa ni kocha wa kipekee, Van Gaal anaweza kufanya vizuri ila katika soka muda na matokeo ndio vitaamua kwamba anafaa au hafai” >>> Chicharito
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
VIDEO YA GOLI LA MECHI YA SIMBA VS TOTO AFRICANS APRIL 17 2016, FULL TIME 0-1