Kuna msemo usemao ‘Kabla Hujafa hujaumbika’ Joyce Kantande ni mwalimu anayefundisha akiwa kitandani kwa takribani miaka 20 sasa kutokana na ulemavu wa miguu alioupata lakini alizaliwa mzima wa viungo.
Ayo Tv na Millardayo.com imeweza kufunga safari hadi Gongo la mboto Majumba Manne na kufanya mahojiano na Mwalimu Joyce ambaye anasema “Ulemavu si Kikwazo cha kutotimiza ndoto zako wala si mkosi”
Ulemavu wake ulitokana na ajali ya gari aliyoipata akiwa na wazazi wake kuelekea mkoani Lindi akiwa na umri wa miaka 7, lakini athari za ajali hiyo hazikuweza kuwa kubwa kwa wakati huo hadi pale alipomaliza Kidato cha 6 na kujiunga na Jeshi.