Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoani Kagera, inawashikilia watumishi wanne, akiwamo askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.
Watu wengine wanaoshikiliwa na Taasisi hiyo ni Askari Polisi na Afisa wa Idara ya Misitu, wote kutoka wilayani Biharamulo.
Akizungumza Mkuu wa TAKUKURU mkoani Kagera, John Joseph, amesema askari huyo wa Jeshi la wananchi alipokea Shilingi 800,000 kati ya shilingi milioni 3, alizoomba kutoka kwa mfugaji mmoja, aliyekamata ng’ombe wake akimtuhumu kuwaingiza katika pori la hifadhi ya Biharamulo.
SERIKALI YAAHIDI KUONDOA URASIMU KATIKA BIASHARA “WATAAMBIWA MASOKO YALIPO”