Ni taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga na kweli imehusisha kifaru cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) saa kumi na moja alfajiri ambapo kifaru kimoja chenye tairi kwenye msafara wa jeshi hilo kimeripotiwa kuacha njia na kugonga nyumba.
Shuhuda alieongea na Power Breakfast ya CloudsFM amesema ‘Imetokea Mnolela kijijini Lindi kwenye msafara huu wa jeshi ilitangulia Iveco moja na nyuma vifaru viwili na walipofika kwenye eneo la shule kuna kona mbaya sana ambayo mara nyingi magari huwa yanaanguka’
‘Kifaru kimoja kwenye huo msafara kilikosa njia na kuingia bondeni kikagonga nyumba ya kwanza kikamkanyaga mwenye nyumba kikagonga nyumba ya pili kikazama kwenye hiyo sebule, kwa harakaharaka waliofariki ni watatu, Wanajeshi watatu na mwenye nyumba ya kwanza na wengine ni majeruhi wa hali mbaya kabisa’
‘Msafara ulikua unatokea Mtwara kuelekea Nachingwea kwenye kambi kuu, hii kona ni kali na aliejenga hii barabara amebakiza baadhi ya changarawe hakufagia kwahiyo mtu akikaribia changarawe zile mtu zinamvuta, hiki kifaru chenye tairi kilikua kwenye spidi kubwa sana usio wa kawaida ikamshinda ndio akatumbukia bondeni’ – Shuhuda
‘Mmoja wa waliofariki ni mama mwenye nyumba ya kwanza ambae alikua amelala kwenye chumba cha mbele ndio alikanyagwa na kufariki papohapo, walioumia ni Wanajeshi waliokua wamekaa juu ya kifaru hicho, wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa Mtwara’ – Shuhuda
Kamanda Mpinga amethibitisha kutokea kwa hili tukio, unaweza kubonyeza play hapa chini kumsikiliza shuhuda mwenyewe na kamanda Mpinga.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB