Tunayo story kutokea kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara ambapo amezungumza mbele ya Waziri wa wizara hiyo, Selemani Jafo kwamba hakuwahi kuwa mtumishi wa serikali bali alikuwa Mwanaharakati mitaani.
Waitara ameyasema hayo leo wakati wa kuwakaribisha Katibu na Naibu Katibu wa wizara hiyo walioteuliwa hivi karibuni ambapo amesema wakati alipofika katika wizara hiyo alijihakikishia kwamba usiku na mchana lazima afanyekazi.
Amesema wizara ya TAMISEMI inafatiliwa kila sekunde, hivyo lazima wawajibike kumsaidia waziri husika kwani wizara hiyo ni pana hasa ukizingatia sekta ya elimu ambayo imekuwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji uangalizi kuzitatua.
“Nyinyi wazoefu, mimi sikuwahi kuwa mtumishi wa serikali nilikuwa mwanaharakati huko mtaani ndio maana najitahidi kujizuia,”amesema.