Leo April 19, 2018 kutoka katika Bunge mjini Dodoma ilikuwa ni siku ya maswali na majibu kwa Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ambapo alitumia nafasi hiyo kutolea ufafanuzi kuhusu kuzuia mahindi kupelekwa nje ya nchi.
Waziri Mkuu Majaliwa Amesema, lengo lao lilikuwa ni kuzuia mahindi ili bidhaa hiyo iongezwe thamani kwa kutengenezwa unga na uweze kuuzwa nje.
“Hata hivyo soko la bidhaa zinazolimwa nchini liko wazi na serikali inafanya kila linalowezekana kuzitafutia masoko.” -Majaliwa