Leo December 20, 2017 President Magufuli alikuwa ni mgeni rasmi katika tukio la uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mjini Dododma ambapo amemwagiza Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango afuatilie suala la hisa za Airtel.
Rais Magufulli ameeleza kuwa kwa taarifa alizonazo ni kwamba Airtel ni mali ya Shirika la Mawasiliano Tanzania yaani TTCL. Inaelezwa kuwa serikali kwenye umiliki wa ndani ya airtel inamiliki kwa ubia wa asilimia 40 kwa 60 na mwekezaji.
“Waziri wa Fedha fuatilia swala la Airtel, kwa taarifa tulizo nazo ni mali ya TTCL palifanyika mchezo wa ovyo, nchi hii ilikuwa ya ajabu, kwa namna hiyo lazima vyuma vitabana tu, tumeamua kubana vyuma vilivyokuwa vimelegea, vilivyokuwa vinahatarisha maisha hasa ya Watanzania masikini,” – JPM
Taarifa kutoka kwenye chombo kimoja cha habari nchini ambayo inatoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inaeleza kuwa uongozi wa juu wa shirika hilo la TTCL imewasilisha hoja kwa serikali ukiitaka idai umiliki wa hisa zote za kampuni ya Aitel TZ, kwani imekuwa ikipunjwa kwenye hesabu za uwekezaji.
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) imefanikisha upasuaji wa kichwa