Watu 28 waliokuwa wanasafiri kutoka Mandera kwenda Nairobi nchini Kenya wameuawa kwa kupigwa risasi eneo la Arabia ambapo Kikundi cha Wapiganaji wa Al Shabaab wamekiri kuhusika na tukio japo Serikali haijathibithisha hilo.
Basi walilokuwa wanasafiria abiria hao lilisimamishwa na kundi la watu hao na kuwaamuru washuke, kisha kuwaua kwa kuwapiga risasi ambapo waliozungumzia tukio hilo wameilaumu Serikali kwa kushindwa kuwapatia usalama watu hao waliouawa.
Naibu Rais William Ruto amesema Serikali imelaani kitendo hicho cha kigaidi huku viongozi wengine wakisisitiza kuwa shambulio hilo halina uhusiano wowote na migogoro ya kidini, mwingine aliejitokeza na kulaani shambulio hili ni kiongozi wa ODM aliyekua waziri mkuu kwenye awamu iliyopita Raila Odinga
Basi hilo lilikuwa na jumla ya watu 60 ambapo wasafiri wengi walikuwa ni walimu waliokuwa wakienda likizo ya sikukuu ambapo katika eneo hilohilo mwezi uliopita kulitokea tukio na maafisa 7 usalama waliuawa.
Kituo cha Televisheni cha K24 TV Kenya kimeripoti taarifa hiyo ambayo nimeirekodi na kukuwekea hapa, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook