Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka Leo June 15, 2018 kwa kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram akimpongeza Mbunge wa CHADEMA, Upendo Peneza.
Zitto ameandika “Mbunge Upendo Peneza anaingia katika rekodi za Wabunge waliotumia nafasi yao kushawishi jambo lenye faida kubwa kwa jamii na likafanikiwa. Serikali imekubali kuondoa kodi ya VAT kwenye Taulo za Kike zinazotumika na Wanawake kwenye hedhi.”
“Kumekuwa na juhudi za kuleta mabadiliko haya miaka mingi kutokana na kazi za Mashirika kama TGNP Mtandao, SNV, Msichana Initiative nk. Upendo, licha ya kuwa na miaka 2 tu Bungeni aliweza kubeba hoja hii na kuiingiza Bungeni na kuunganisha Wabunge wote kutoka Vyama vyote.” ameandika Zitto
“Licha ya kwamba kampeni yake ilikuwa ni Watoto wa shule wapewe Taulo hizi bure ( litafika tu hilo kupitia mamlaka za Serikali za Mitaa ), amepata mafanikio makubwa kwa uamuzi wa Serikali kuondoa VAT na hivyo kushusha gharama za Taulo hizi. Upendo ameacha alama ( legacy).” Zitto Kabwe
“Mzee William Shelukindo aliwahi kunieleza tofauti ya kuwa Mbunge ( Member of Parliament ) na Mwana Bunge ( a parliamentarian). Kwamba Mwana Bunge ni Mbunge ambaye anaacha alama Katika kazi zake za Bunge na kwamba anaweza kuunganisha wabunge bila kujali Itikadi za Vyama Katika Hoja zenye maslahi ya Umma.”
“Alinieleza haya wakati ananipongeza kuhusu Hoja ya Buzwagi ambayo ndiyo iliyoleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya Madini.”
“Upendo Peneza sasa amepanda daraja kutoka kuwa Mbunge na kuwa Mwana Bunge, a Parliamentarian. Hongera sana Upendo Peneza Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Geita ( CHADEMA ) kwa kutendea haki nafasi yako na kufanikisha harakati za wanawake. Umeipa Bajeti ya mwaka 2018/19 taswira ya BAJETI YA KIJINSIA” alimaliza Zitto Kabwe
LIVE MAGAZETI: Watapigwa kipigo cha Mbwa koko!, Bajeti yang’ata yapuliza