Kuna hii ya kuifahamu leo June 21, 2018 ni kumhusu Rais wa Marekani Trump ambapo amesitisha utekelezaji wa sera yake ya kuwatenganisha Watoto wa Wahamiaji na Wazazi wao katika mpaka wa nchi yake na Mexico.
Taarifa hii inakuja tu baada ya Watu wengi kupinga vikali sera hiyo ya Rais Trump akiwemo Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis akisema kuwa sera hiyo sio mwarobaini wa tatizo la Wahamiaji duniani..
Aidha imeelezwa kuwa sio Papa tu aliyempinga Rais Trump bali hata Bunge, makundi ya haki za binadamu, mkewe Trump pamoja na wake wa marais wastaafu wa nchi hiyo wamepinga vikali sera hiyo ya Trump.
Hata hivyo Rais Trump amesema kuwa ijapokuwa amesitisha utekelezaji wa sera hiyo bado ataendelea kuilinda mipaka ya nchi yake ya Marekani.