Baada ya kucheza mchezo wao wa kwanza nyumbani wa hatua ya Makundi wa CAF Champions League kwa Simba dhidi ya JS Saoura na kuvuna point tatu na ushindi wa magoli 3-0, Simba SC ilifuatia kwa kucheza michezo yao ya miwili ya michuano hiyo ugenini, baada ya kupoteza 5-0 dhidi ya AS Vita katika jiji la Kinshasa DRC, Simba ikaenda Alexandria Misri kukipiga dhidi ya Al Ahly na kujikuta ikipokea kipigo kingine tena cha magoli 5-0.
Tumekuwa tukisikia mambo mengi juu ya hujuma za waarabu au mbinu za hapa na pale ili wapate ushindi lakini kingine tulisikia kuwa Al Ahly waliipeleka game ya Simba SC dhidi yao katika mji wa Alexandria kwakuwa unabaridi, so tumepiga stori na staa wa soka wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadid ya nchini Morocco na kumuuliza mipango ya timu za kiarabu wanapocheza soka na timu za kimataifa.
Unajua msuva yeye anacheza Morocco na Simba wao walienda kucheza Misri ila tunajua kuwa nchi za kiarabu au soka la timu za Afrika Kaskazini zinafanana sasa vipi kwa upande wao maandalizi gani huwa wanafanya kuelekea mechi za kimataifa? kama mwaka jana tuliona walicheza na AS Vita katika mji wa Kinshasa, Msuva amesema kuwa timu hizo huwa zinatuma watu mapema wachunguze kila kitu chao.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF