Chama cha soka England FA leo kimetangaza rasmi kufikia maamuzi ya kuwaomba msamaha wachezaji Chris Smalling wa Man United na mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane kufuatia tweet yao waliyoipost kupitia account yao ya twitter kutafsirika tofauti.
FA wameomba radhi kufuatia jumbe wao waliopost baada ya mchezo wa nusu fainali ya FA kati ya Tottenham dhidi ya Man United uliyomalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-1, ambapo ujumbe huo unatafsirika kama ulimkosea heshima Harry Kane na Smalling.
Tweet yao ilikuwa inasomeka “Nini kipo mfukoni mwako” halafu inaonekana Smalling anajibu ni “Harry Kane” kitu ambacho kilitengenezwa kwa lengo la utani tu wakimaanisha kuwa Smalling amefanikiwa kumdhiniti Harry Kane katika mchezo dhidi yao.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao