“Niliwaombe ndugu zangu wa TAKUKURU kumekuwepo na wizi mkubwa sana kwenye eneo letu la Madini Manyara na taarifa hizi sio siri tena ukifika Arusha unapata taarifa ni namna gani wizi unaendelea na rushwa imekuwa ikitamaraki katika eneo hili” Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohammed Mchengerwa
“Sasa niwaagize TAKUKURU nawapa wiki mbili ili muende mkafanye uchunguzi kile kinachoendelea kule Mererani katika mgodi ambao unamilikiwa na serikali na wizi mkubwa unaoendelea kutokana na taarifa ambazo zimeenea katika Mikoa ya Arusha na Manyara ili tuweze kubaini ni kitu gani kinaendelea katika mgodi wetu,” amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohammed Mchengerwa, wakati akizindua program tumishi ya Ajira App uliofanyika leo Novemba 19, 2021 jijini Dodoma.