Headlines za David Kafulila wa Chama cha NCCR– Mageuzi kuamua kufika Mahakama kuu ya Tabora kuhusu sababu ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu kuonesha hakupata Kura za kutosha ili awakilishe wananchi wa Kigoma Kusini.
Sasa kilichoendelea ni kwamba Mahakama Kuu kanda ya Tabora imemua Kafulila kulipa Milioni 7.5 badala ya Milioni 15 kama dhamana ya kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi katika jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa Husna Mwilima,Mkurungezi wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza, msimamzi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
‘Leo mahakama kuu ya Tabora shauri langu la ombi la kukadiria la kugharamia kama dhamana ya kesi lilisikilizwa kwa mara ya mwisho, kwa sababu lilianza kusikilizwa jana na leo jaji aliweza kuamua baada ya kuzingatia pande zote mbili na kusema nilipe kiasi cha Milioni 7.5 badala ya shilingi milioni 15 ambayo ilikuwa imepangwa na mwanasheria wa Serikali pamoja na wakili wa Husna Mwilima’ -David Kafulila
‘Katika kesi hii washtakiwa ni Husna Mwilima pamoja na msimamizi wa Uchaguzi kwa hiyo katika utaratibu wa kawaida kwamba mtu anapofunguka kesi ya Uchaguzi anatakiwa alipe dhamana isiyozidi milioni 5 kwa kila anayemshtaki…. kwahiyo katika hali kawaida maana yake ningelipa milioni 15 lakini kwa mujibu wa sheria ni uamuzi wa jaji kuamua kama anayeshtakia alipe kiasi gani au anaweza asilipe kiasi chochote‘>>> – David Kafulila
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza David Kafulila
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.