Kaimu Mkuu Idara ya Ardhi Wilaya ya Chalinze Ndg. Deo msilu amewapongeza Wananchi wa Wilaya ya Chalinze Kata za Pera na Bwilingu kwa Kuupokea Mradi wa Uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Nchini (LTIP) ambao umeweza kuhakiki vipande 11,000 vya ardhi ambapo wameweza kupima na kuvuka lengo la kupima vipande 10,000 kwa miezi sita huku lengo kuu likiwa ni kufikia vipande 50,000.
Hata hivyo Wananchi katika Halmashauri ya Mji mdogo wa Chalinze wameiomba Serikali kuwafikia katika maeneo mengine ambayo bado hayajafikiwa na mradi huo ili kupunguza migogoro ya ardhi, ujenzi holela na pia kuondokana na imani za Kishirikina.
Aidha Mradi huo tayari umezifikia Kata mbili kati ya 15 Wilayani humo ambapo utekelezaji wake umeonesha mafanikio makubwa sana kwa kuweza kutatua idadi kubwa ya migogoro pamoja na kuanziasha barabara nyingi za mitaani ambazo hazikuwepo hapo mwanzo jambo ambalo lilikua linakwamisha baadhi ya shuguli za kijamii katika mitaa.