Jumapili ya December 17 2017 ndio siku ambayo kiungo wa kimataifa wa Brazil Ricardo Kaka alitangaza rasmi kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 35, Ricardo Kaka ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa anaitumikia club ya Orlando City ya Marekani.
Kama humfahamu Ricardo Kaka ni staa ambaye amewahi kucheza vilabu mbalimbali Ulaya kama AC Milan na Real Madrid lakini Kaka ndio mchezaji pekee aliyewahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or mbele ya Ronaldo na Messi mwaka 2007.
Kaka pia ndio mchezaji wa mwisho wa Brazil kuwahi kushinda Ballon d’Or, kama humfahamu Ricardo Kaka alizaliwa 1982 Gama Brazil jina lake kamili ni Ricardo Izecson dos Santos, baba yake alikuwa ni civil engineer na mama yake alikuwa mwalimu.
Familia aliyokuwa anatokea kaka ilikuwa ipo vizuri kiuchumi kitu ambacho kilimfanya awe na uwezo wa kumudu kusoma na kucheza mpira jina la Kaka ni la utani na halina maana yoyote katika lugha yao ya kireno, lilipatikana enzi za utoto ambapo mdogo wake Rodrigo kushindwa kutamka neno Ricardo.
Ricardo Kaka akiwa na umri wa miaka 18 alipata majaribu ambayo yangeweza kugharimu maisha yake ya soka kwa kuumia uti wa mgogo baada ya kuruka katika swimming pool, hali yake ilikuwa inatajwa kuwa na uwezekano mdogo sana wa kupona lakini kwa uwezo wa Mungu alipona.
Mstaafu Kikwete na Zitto Kabwe baada ya Zanzibar kuingia fainali