Tumekuwa tukiyasikia matukio ya ukatili wa kijinsia limekuwa likichukua headline katika maeneo mbalimbali ya Tanzania, sasa limefika hadi Bungeni wakati Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ilipowasilisha hotuba ya bajeti yake ya mwaka 2016/2017
Katika kipindi cha michango ya Wabunge kuhusu hotuba hiyo Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa alisiamama Bungeni na kusema….
>>’Suala la ujatili wa kijinsia limekuwa kubwa, tulitembelea gereza la Segerea tumekuta wasichana wa miaka 14,13 ambao walikuwa mahouse girl wa watu. Chakushangaza wale watoto wamefungwa miaka miwili kwa kosa la kuchana dela la bosi wake ‘
‘Hawa watoto hawana makosa, wakifika kule gerezani wanakutana na waharifu wa kweli na wakikaa kule miaka miwili wakitoka wanakuwa wamejifunza uharifu ‘
Kaluwa hajaliacha pia hili la Wanawake…’Naishukuru Serikali kwa kuanzisha Benk ya Wanawake mwaka 2009, lakini haisaidii wanawake walengwa bali inasaidia wale wenye pesa zao‘
‘Kuna wakinamama wanahitaji hata elfu 50 ya mtaji aweze kupika vitumbua au chapati hajui kwa kuzipata, nimuombe Waziri na Mkurugenzi waangalie watawafuata vipi wakinamama waliopo mitaani ili waweze kusaidika‘
Unaweza kumsikiliza Kaluwa akichangia kwenye hii video…
ULIIKOSA HII WIZARA YA AFYA IMEWASILISHA BAJETI YAKE YA BILIONI 845?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE