Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa wanawake wanaotoka mikoa ya kusini wanazaa watoto wachache zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine. Aidha utafiti huo umetaja kuwa wanawake wa Dar es salaam wanazaa wastani 3.8 mpaka 4.2 ikilinganishwa na mikoa mingine ya Kagera, Kigoma ambayo huzaa wastani wa watoto 6.8.
AyoTV na millardayo.com imempata Dk. Heri Tungaraza kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili kaeleza sababu zinazopelekea wanawake wa DSM kuwa na watoto wachache ikilinganishwa na mikoa mingine.
‘imechangiwa sana na namna familia zetu ambavyo zimejitahidi kufanya uzazi wa mpango, watu wameamua kupunguza idadi ya watoto kimakusudi kutokana na sababu za uelewa na kutaka kubadilisha staili za maisha’-Tungaraza
VIDEO: Jeshi la Polisi limetangaza magari mapya yatakayoruhusiwa kubeba abiria, Bonyeza play hapa chini kutazama