Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila mewataka Vibaka wanaokaba na kupora Watu kwenye eneo la Daraja la Selander kuacha mara moja na kutoa rai kwamba kuna Mtu amechoka kuishi mtaani na akaona eneo hilo ndio pahali pazuri pa kuishi yatamkuta ya kumkuta.
Chalamila amesema hayo alipotembelea eneo la daraja hilo lililo karibu na msitu wa mikoko leo ambako Wahalifu hujificha “Tumetembelea hapa kuangalia usalama wa Raia, waache mara moja masuala ya kuumiza Watu na kukwapua mali za Watu, nalipongeza Jeshi la Polisi asilimia kubwa ya waliokuwa wanafanya uhalifu wamekamatwa, Baba au Mama chunga Kijana wako asije akang’aa kwenye msitu huu na makubwa yakamkuta akiwa bado mdogo”
Katika ziara hiyo RC Chalamila aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala @mpogoloe na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM Muliro Jumanne.